Friday, November 4, 2011

..KAMPENI YA CHANJO INAZIDI KUSONGA MBELE

Dodoma Mwl. Nyerere Square chanjo ilitolewa hapo.

"karibuni sana mtoe chanjo ya rushwa"

"kijijini Mpui chanjo imefika"

Pokeeni chanjo mkawaambie na wengine 'rushwa ni adui wa haki na maendeleo'.

'nimewachagulia huyu, awe Tambiko la chanjo'

Ahsante sana!

Hapa ndipo alipozaliwa Vitali Maembe miaka 35 ilopita kijini Mwazye, chanjo imefika hapa

Habari za asubuhi?
Onyesho la Kwanza kijijini Msoma,Ilikuwa siku ya Jumapili baada ya Ibada, wanakijiji waliudhuria kwa wingi kupata Chanjo dhidi ya Rushwa, Uvivu na Ubinafsi.

Taa hii ilitoa nuru na mwanga kwa usiku wote wa siku a kwanza kuwasili kijijini Msoma, nuru yake ilifanikisha kufanyika kwa Tambiko la kuomba na kubariki safari  na Kazi nzima ya Chanjo dhidi ya Rushwa, Uvivu na Ubinafsi.

 

       Kwa mila nyingi za kiafrika mgeni hukirimiwa kwa kinywaji kama ishara ya upendo na ukarimu. Kijijini Msoma timu ya Chanjo ilikaribishwa kwa kinywaji cha Asili ‘KOMONI’ kama sehemu ya ukarimu na pia kama sehemu ya Tambiko komoni ilitumika kama mbadala wa Chimpumu pombe ya asili ya eneo hilo, hii ilikuwa kuwakaribisha wageni na kuwaombea heri katika safari ndefu ya mapambano dhidi ya Rushwa.


4.     Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria Chanjo dhidi ya Rushwa, Uvivu na Ubinafsi kijijini Msoma, Sumbawanga Vijijini.



 Mmoja wa watu waliovutiwa na Muziki pamoja na Ujumbe unaoelimisha kuhusu Rushwa Kijijini Mwazye, Sumbawanga vijijini, hii ilikuwa ni sehemu ya onyesho la Chanjo dhidi ya Rushwa, Uvivu na Ubinafsi.


 Japokuwa alikuwa na hamu kubwa ya kusikiliza muziki, lakini ‘kucheza muziki’ ni jambo ambalo watu wengi wa maeneo ya vijijini hukosa fursa hiyo, kuwepo kwa onyesho la Chanjo kuliwapa fursa wanakijiji wa Mwazye kuelimika kuhusu Rushwa na kupata wasaa wa kuburudika na Muziki pia.
                                             Watu waliohudhuria onyesho la Chanjo kijijini Mwazye.


Vitali Maembe akitoa Chanjo dhidi ya Rushwa, Uvivu na Ubinafsi kwa wanakijiji waliohudhuria Onyesho hilo kijijini Mwazye.

Sehemu kubwa ya zoezi zima la safari ya Chanjo ya Rushwa ni kujenga jukwaa la majadiliano linalowezesha wanaharakati wa Chanjo kuweza kufanya majadiliano ya wazi kuhusu Rushwa na matatizo yanayoletwa nayo. Msanii Vitali Maembe akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa majadiliano, Kijijini Mwazye.





Kucheza kwa furaha huku ukitoa ujumbe kuhusu Rushwa kunashawishi Umma kuamini kuwa Rushwa si Mwiko kuijadili, njia mbali mbali zinaweza kutumika kuweza kufikisha ujumbe mojawapo ikiwa sanaa asilia.Vitali Maembe akicheza mojawapo ya ngoma za asili, Sumbawanga.


1.    Kuimba pamoja na hadhira wimbo unaofahamika zaidi kunajenga hamasa ya kushiriki katika majadiliano, zoezi mojawapo kubwa katika safari ya Chanjo ni kuishawishi hadhira kuwa mapambano dhidi ya Rushwa hutakiwa kufanyika katika Umoja wetu. Msanii Vitali Maembe akiimba pamoja na hadhira mojawapo ya nyimbo maarufu kijijini Mwazye.

No comments:

Post a Comment