Thursday, April 19, 2012

SAFARI YA CHANJO MIKOA YA KUSINI MWA TANZANIA

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutulinda nakutupa mema mengi ambayo tunayajua na tusiyoyajua, ametujaalia kumaliza mzunguko wa maonesho ya Chanjo ya Rushwa kwa nchi nzima.
Tarehe 27/03/2012 tuliianza safari ya mikoa ya kusini na sasa tumemaliza na kutimiza lengo letu la kuifikia nchi nzima.

Muda si mrefu tutaanza maonesho nane maalumu ya kuhitimisha Chanjo, pia itakuwa ni sehemu ya taarifa kwa wananchi, wanahabari na wote wenye haja ya kujua zaidi kuhusu chanjo.
Pindi utakapopata ratiba usisite kukaribia.

‘Taifa litajengwa na wenye moyo’

Watoto wa shule, naipanga- nachingwea. ‘tunakwenda shule na majembe, sio adhabu wala si tabu tunajifunza mengi, kila mwaka wakati kama huu huwa tunaagiza majembe, tunayatumia wenyewe. wazazi wetu hawashangai. ilatunapo agizwa pesa ya makuti ndipo inakuwa kero’.



  Toka tunduru kwenda songea, barabara ni mbovu,bado hili ni tatizo kubwa kwa mikoa ya kusini wengine wanasema ‘tunaona tu vibao vya kutngeneza barabara lakini mpaka vinaoza,     matengenezo hatuyaoni’  ‘sisi huko kulima ndio tumeacha tunalima kiasi cha chakula tu lakini ukizidisha hapo utasafirisha vipi viwafikie wateja?’ tulipojadiliana nao wanasema hii yote nisababu ya rushwa kushamiri nchini.

        ‘Sio kwamba hatupati baba, tunapata lakini tangu walipokuja kukopa korosho zetu mpaka leo hawajatulipa, na hao wawakilishi wetu wakienda huko kufuatilia wanatulizwa na rushwa wanarudi huku na maneno ya faraja lakini hali ndio kama mnavyoiona, hatujui hata tuwafungashie nini wanangu mwende nacho nanyi mfurahi’




Hii ndiyo barabara ya kuelekea mikoa ya kusini kupitia kilwa. ‘usione tunabeba mikate mingi ukazani kwetu ni washamba sana au hatuna bekari, hii ni tahadhari tu, huku kulala siku mbili tatu sio ajabu  barabara hii ilitakiwa iwe imekamilika lakini rushwa tu kaka! Malendikruza yao


Kiapo! ‘Rushwa ni adui wa haki namaendeleo!  Naapa kwamba sitamshawishi mtu kushiriki rushwa, nitaweka juhudi katika masomo ili nisiitegemee rushwa katika kubabaishi ili niishi, sitaiacha nafsi yangu iangukie katika rushwa. Kwaajili yangu na taifa langu, Mungu nisaidie!’