Wednesday, July 4, 2012

...WANA WA BAGAMOYO WALIVYOPEWA CHANJO

Wananchi waliofurika kutoka sehemu mbalimbali za Bagamoyo na nje ya Bagamoyo ili kupewa Chanjo ya Rushwa kutoka kwa Vitali Maembe na Bendi ya The Spirits


 Baadhi ya washiriki walikuwa ni wadau wa karibu kutoka shirika la SPIDER kutoka Sweden

 "Hata mtoto naye ana kipaji"
Hapa mtoto akionyesha umahiri wa kucharaza gitaa la bezi katika onyesho la kutoa Chanjo Ya Rushwa siku ya Jumamosi ya tarehe 30 Julai

"Asante sana Vitali"
Hapa Paula kutoka SPIDER akimpongeza Vitali Maembe kwa kufanya mapambano dhidi ya rushwa kupitia Chanjo Ya Rushwa

Baadhi ya wasanii walioshiriki katika kutoa Chanjo ndani ya Bagamoyo

Bendi ya The Spirits wakionyesha umahiri katika kutoa ujumbe ulioambatana na burudani ndani yake kuhusiana na rushwa

Vitali Maembe akiimba pamoja na waliohudhuria tamasha hilo la bure mjini Bagamoyo

Wednesday, June 20, 2012

.....CHANJO ILIVYOHAMASISHA WENGI


....Simu ilitumika na wengi kuchukua picha na video za tukio..


 Washiriki wa onesho la Chanjo wakifuatilia kwa umakini ujumbe unaotolewa





Vitalis akifafanua jambo wakati wa Onyesho la Chanjo Ya Rushwa


Sunday, May 20, 2012

CHUO CHA SLADS BAGAMOYO WAPEWA CHANJO...

Vitali Maembe akigawa CHANJO YA RUSHWA kwa wanafunzi wa SLADS BAGAMOYO

Mwl. Mwalubawa akifanya utambulisho kwenye onesho maalumu la Chanjo ya Rushwa  Chuoni kwake SLADS Bagamoyo.



 ulimwengu wa teknolojia ulijirihirisha, wengi walichukua kumbukumbu katika simu zao za mikononi.
ulimwengu wa teknolojia ulijirihirisha, wengi walichukua kumbukumbu katika simu zao za mikononi.

Monday, May 7, 2012

..CHANJO KWA KILA RIKA

Vitalis Maembe akitoa CHANJO YA RUSHWA kwa wakazi wa Mti Mwiba-Masasi.

Hadi watoto nao wanastahili kupewa CHANJO YA RUSHWA, hapa ni Lizabon-songea

Vitali akiwa anahamasisha jambo ndani ya Masasi.

"si barabara zote ni mbaya...ila kwingine ni VIONGOZI TU"




Tuesday, May 1, 2012

..HARAKATI ZA CHANJO YA RUSHWA ZAPENYEZA HADI VIJIJINI

                                             Chanjo ikitolewa kwa wana wa SONGEA

                                               ............................elimu ni ukombozi

                         wananchi wa rika mbalimbali wakipata nasaha za maisha kupitia CHANJO..

                           hapa ni kilwa kivinje, bado tunasisitiziwa hatari ya ugonjwa huu, ukimwi bado



'huu ni wakati pekee ambao tunaweza kuikoa nchi yetu kwa sauti na kalamu zetu

Thursday, April 19, 2012

SAFARI YA CHANJO MIKOA YA KUSINI MWA TANZANIA

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutulinda nakutupa mema mengi ambayo tunayajua na tusiyoyajua, ametujaalia kumaliza mzunguko wa maonesho ya Chanjo ya Rushwa kwa nchi nzima.
Tarehe 27/03/2012 tuliianza safari ya mikoa ya kusini na sasa tumemaliza na kutimiza lengo letu la kuifikia nchi nzima.

Muda si mrefu tutaanza maonesho nane maalumu ya kuhitimisha Chanjo, pia itakuwa ni sehemu ya taarifa kwa wananchi, wanahabari na wote wenye haja ya kujua zaidi kuhusu chanjo.
Pindi utakapopata ratiba usisite kukaribia.

‘Taifa litajengwa na wenye moyo’

Watoto wa shule, naipanga- nachingwea. ‘tunakwenda shule na majembe, sio adhabu wala si tabu tunajifunza mengi, kila mwaka wakati kama huu huwa tunaagiza majembe, tunayatumia wenyewe. wazazi wetu hawashangai. ilatunapo agizwa pesa ya makuti ndipo inakuwa kero’.



  Toka tunduru kwenda songea, barabara ni mbovu,bado hili ni tatizo kubwa kwa mikoa ya kusini wengine wanasema ‘tunaona tu vibao vya kutngeneza barabara lakini mpaka vinaoza,     matengenezo hatuyaoni’  ‘sisi huko kulima ndio tumeacha tunalima kiasi cha chakula tu lakini ukizidisha hapo utasafirisha vipi viwafikie wateja?’ tulipojadiliana nao wanasema hii yote nisababu ya rushwa kushamiri nchini.

        ‘Sio kwamba hatupati baba, tunapata lakini tangu walipokuja kukopa korosho zetu mpaka leo hawajatulipa, na hao wawakilishi wetu wakienda huko kufuatilia wanatulizwa na rushwa wanarudi huku na maneno ya faraja lakini hali ndio kama mnavyoiona, hatujui hata tuwafungashie nini wanangu mwende nacho nanyi mfurahi’




Hii ndiyo barabara ya kuelekea mikoa ya kusini kupitia kilwa. ‘usione tunabeba mikate mingi ukazani kwetu ni washamba sana au hatuna bekari, hii ni tahadhari tu, huku kulala siku mbili tatu sio ajabu  barabara hii ilitakiwa iwe imekamilika lakini rushwa tu kaka! Malendikruza yao


Kiapo! ‘Rushwa ni adui wa haki namaendeleo!  Naapa kwamba sitamshawishi mtu kushiriki rushwa, nitaweka juhudi katika masomo ili nisiitegemee rushwa katika kubabaishi ili niishi, sitaiacha nafsi yangu iangukie katika rushwa. Kwaajili yangu na taifa langu, Mungu nisaidie!’

Friday, March 23, 2012

..CHANJO KUELEKEA KUSINI..

 Timu ya CHANJO inatarajariwa kusafiri jumapili kuelekea mikoa ya KUSINI MWA TANZANIA kukamilisha mzunguko wa maonesho ya muziki nchi nzima.

The Spirits watakuwa wakiimba na kutoa nafasi ya majadiliano kuhusu namna ya kuidhibiti rushwa.

Maeneo yatakayofikiwa ni pamoja na Mtwara, Masasi, Lindi, Songea na Mahenge na baada ya maonesho hayo itarudi Bagamoyo kuendelea na Chanjo Maalum kwa vyombo vya habari na Vyuo Vikuu.


Mapambano ya Ukombozi yanaendelea.