Wednesday, December 28, 2011

CHANJO ILIVYOKONGA WANANCHI MIKOANI


 1. Mwitongo-Butiama nyumbani kwa Mwl.Nyerere, Hili ni jiwe ambalo Mwenge mkubwa huwasha hapo kila mwaka. Vitali Maembe akionesha ishara ya mafanikio juu ya jiwe la Mwenge, alisema ni baraka kubwa kufika hapo yeye na timu nzima ya Chanjo ya Rushwa, iliwachukuwa muda mrefu na nguvu nyingi kufika hapo, vikwazo  vingi vilitokea lakini hawakukata tamaa. chanjo inaendelea

 2. Maswali na majibu kuhusu Chanjo
3. Wengine wanashangazwa na aina hii ya ujumbe na mtindo wa uwakilishaji, watu wa njoro Moshi wanauliza kutaka kujua kwanini Chanjo imekuja kwao na kwanini imeletwa na The Spirits na sio Serikali.
 4. Wengine hawakupenda kusogelea lakini kwa umbali waliokaa walisema wameipata vizuri.
 5. Wakaazi wa kijiji cha Butiama wakisikiliza kwa makini huduma ya Chanjo iliyotolewa kwao na wanamuziki wa The Spirits

6. Wanawake wa Pangani mkoani Tanga wakivunja ukimya juu ya mateso wanayoyapata kama wanawake pale Rushwa inapopewa nafasi hasa katika huduma za kijamii.
7. Vitali Maembe na Wananchi wa Sakura wakijadiliana kuhusu Rushwa 

 8. Watoto waliguswa sana na Chanjo lakini kwa namna ambayo tunaweza tusiijue, inawezekana sana wakawa wameguswa na kuvutwa na mlio mkubwa wa muziki na utamu wa mapigo yake, kilichotokea ni kwamba walihudhuria, walicheza na kufurahi, Chanjo ilikuwa na umuhimu wa aina yao kwao. Walipata Chanjo.
 9. Hapa ilikuwa Njoro, mkoani Kilimanjaro, walipata chanjo na kufurahia lakini ujumbe wa namna hii uliwashangaza
 10. Siku hii watu walinogewa na kusema 'Chanjo imetuvuta wengi nasi tunatamani kutoa Chanjo'

 11. Wakaazi wa Pangani wakihudhuria onesho la Chanjo, hili lilikuwa onesho maalum baada ya watu kuomba tena kupewa chanjo kwa mara ya pili siku ya kwanza haikuwatosha.
 12. Watoto kwa wakubwa wakipata Chanjo Kituo cha mabasi wilaya ya Pangani mkoani Tanga
 13. Wananchi waliutumia vema ujio wa Chanjo, walisema kila kigumu kilicholetwa na Rushwa
14.  Safari Chanjo ilihudhuriwa na Wakinamama na wanawake wengi, lakini wachache sana walizungumza na kuuliza maswali wakati wa majadiliano, wengi walisikiliza na kutafakari wenyewe mioyoni mwao, na baadaye walijadiliana wao kwa wao. Inawezekana kabisa kuwa malezi na tamaduni na taratibu zetu zinachangia haya. Chanjo inaendelea na mchango wao tunauona.

 15. Chanjo wakati mwingine ilikuwa ni kama kitu cha kushangaza, lakini kimewavutia.
16. Watoto waliguswa sana na Chanjolakini kwa namna ambayo tunaweza tusiijue, inawezekana sana wakawa wameguswa na kuvutwa na mlio mkubwa wa muziki na utamu wa mapigo yake, kilichotokea ni kwamba walihudhuria, walicheza na kufurahi, Chanjo ilikuwa na umuhimu wa aina yao kwao. Walipata Chanjo.
 17. Salumu Mpute akicharaza Bass huku akisikilizwa na watu kwa makini wakati Spirits ikitoa chanjo.
18. Watoto waliguswa sana na Chanjolakini kwa namna ambayo tunaweza tusiijue, inawezekana sana wakawa wameguswa na kuvutwa na mlio mkubwa wa muziki na utamu wa mapigo yake, kilichotokea ni kwamba walihudhuria, walicheza na kufurahi, Chanjo ilikuwa na umuhimu wa aina yao kwao. Walipata Chanjo.
19. Wananchi walikula kiapo baada ya kupata Chanjo, Kiapo hufanyika mara mbili mwanzo wa onesho na baada ya majadiliano, hiki huwa ni kipimo bora cha kujua kama watu wameelewa.
20. Safari Chanjo ilihudhuriwa na Wakinamama na wanawake wengi, lakini wachache sana walizungumza na kuuliza maswali wakati wa majadiliano, wengi walisikiliza na kutafakari wenyewe mioyoni mwao, na baadaye walijadiliana wao kwa wao. Inawezekana kabisa kuwa malezi na tamaduni na taratibu zetu zinachangia haya. Chanjo inaendelea na mchango wao tunauona.

21. Bw. Makame akifafanua ukimya wa watu 'Watu wanashindwa kusema lakini wanaumia, watu wanapatashida kwenye kupata kazi na nafasi katika mashamba ya Mkonge huku Sakura na sehemu nyingine hapa Tanga, lakini wanaogopa kusema au kulalamika kwakua mkiondoka hapa watanyanyasika kwakuwa wamesema ukweli'
22. Siku ya mkesha wa Uhuru, watu waliokusanyika katika kiwanja cha michezo cha Babati mkoa wa Manyara walipata fursa ya kupewa Chanjo. Waliipokea na kushiriki vema.
23. Baadhi ya watalii walioitembelea Tanzania walipata bahati ya kupata Chanjo. Walishiriki na wenyeji jukwaa moja.
24. Timu ya Chanjo ilipofika Butiama ilimtembelea Chifu wa sasa wa wazanaki, Mzee Wanzagi aliwakaribisha vizuri na kuwaelezea jinsi Mwl. Nyerere alivyoipenda nchi yake na kuichukia Rushwa.
25. RUSHWA NA EWURA, Mafuta machafu na yenye maji mengi kutoka katika vituo vya mafuta vilivyothibitishwa. Wanamuziki wa Chanjo wakishusha Tenki la mafuta la gari kumwaga mafuta, iliwalazimu kufanya hivyo zaidi ya mara tatu katika safari. na kutembea mwendo mrefu kwa miguu na pikipiki kutafuta mafuta ya 'videbe' yaliyo salama ili kuendelea na Safari.


No comments:

Post a Comment