Wednesday, July 4, 2012

...WANA WA BAGAMOYO WALIVYOPEWA CHANJO

Wananchi waliofurika kutoka sehemu mbalimbali za Bagamoyo na nje ya Bagamoyo ili kupewa Chanjo ya Rushwa kutoka kwa Vitali Maembe na Bendi ya The Spirits


 Baadhi ya washiriki walikuwa ni wadau wa karibu kutoka shirika la SPIDER kutoka Sweden

 "Hata mtoto naye ana kipaji"
Hapa mtoto akionyesha umahiri wa kucharaza gitaa la bezi katika onyesho la kutoa Chanjo Ya Rushwa siku ya Jumamosi ya tarehe 30 Julai

"Asante sana Vitali"
Hapa Paula kutoka SPIDER akimpongeza Vitali Maembe kwa kufanya mapambano dhidi ya rushwa kupitia Chanjo Ya Rushwa

Baadhi ya wasanii walioshiriki katika kutoa Chanjo ndani ya Bagamoyo

Bendi ya The Spirits wakionyesha umahiri katika kutoa ujumbe ulioambatana na burudani ndani yake kuhusiana na rushwa

Vitali Maembe akiimba pamoja na waliohudhuria tamasha hilo la bure mjini Bagamoyo