Monday, October 31, 2011

Chanjo Tour;

Rushwa ni kama giza lililotanda kwenye fikra na mioyo yetu. Maeneo mengi ya vijijini hakuna huduma ya Umeme, Kibatari (Koroboi) hutumika kulifukuza giza na kuleta nuru na mwangaza. Ujio wetu kijijini Msoma ulipokelewa na Koroboi ikimulika eneo lote kama taa itoayo nuru na ishara ya kuleta tumaini mahali penye giza nene. Safari ya Chanjo nchini kote imeanzia hapa, kwa mwanga mdogo uangazao mahali pote.

Thursday, October 20, 2011

TIMU YA CHANJO YAZIDI KUCHANJA MBUGA KILA PEMBE..

Gari linalobeba wanamuziki katika kusambaza CHANJO likiwa limefika Chuo Kikuu Dar Es Salaam tayari kugawa Chanjo kwa Wasomi

Wanamuziki wa kundi la THE SPIRITS wakiwa katika moja ya safari ya kuelekea kugawa CHANJO YA RUSHWA Tanzania. 

Tuesday, October 18, 2011

...ILIVYOKUWA MTONI MTONGANI-DAR

Vitali Maembe na The Spirits wakigawa Chanjo kwenye onyesho lilifanyika Mtoni Mtongani,Dar Es Salaam

"Watoto ni Kizazi Cha Kesho na Wanastahili Chanjo"...Watoto pia walipewa Chanjo, na watu wazima pia walikuwepo katika kushiriki Onyesho la ugawaji wa Chanjo kutoka kwa Vitali Maembe na The Spirits.